VIBARUA WANAHITAJIKA(Elimu ya Form Four) -NAFASI 62 ZA KAZI TUME YA MADINI

TANGAZO NAFASI ZA KAZI (WAKAGUZI WASAIDIZI WA MADINI UJENZI NA VIWANDANI) 
UTANGULIZI

Tume ya Madini ni Taasisi iliyo chini ya Wizara ya Madini yenye jukumu la kusimamia shughuli za Madini nchini. Lengo kuu la Tume ni kuboresha usimamizi na udhibiti katika ukaguzi wa uzalishaji na biashara ya madini. Pia,Tume ina jukumu la kuhakikisha Sera, Sheria, Kanuni na taratibu zinazoongoza shughuli za Madini zinafuatwa ipasavyo ili kuongeza pato la Taifa kutoka katika sekta ya Madini.

Baadhi ya majukumu ya Tume ya Madini:-
i. Kusimamia na kuratibu kikamilifu utekelezaji wa sheria na kanuni za Madini;
ii. Kusimamia na kudhibiti kwa ufanisi biashara ya Madini ili kuongeza mchango wa Sekta ya Madini kwenye pato la Taifa;
iii. Kusimamia utafutaji na uchimbaji endelevu wa rasilimali madini;
iv. Kutoa, kusitisha na kufuta leseni pamoja na vibali kulingana na Sheria,Kanuni za Madini;
v. Kuchambua na kuthaminisha madini yaliyozalishwa na migodi mikubwa ,ya kati na midogo ili kuwezesha ukusanyaji wa mrabaha stahiki;
vi. Kufuatilia na kuzuia utoroshaji /magendo ya madini, na ukwepaji wa ulipaji mrabaha kwa kushirikiana na vyombo na Mamlaka nyingine husika za Serikali; na
vii. Kuandaa na kutoa bei elekezi za Madini mbalimbali kutokana na bei za soko za hapa nchini na za kimataifa.

NAFASI ZA KAZI
Tume ya Madini inawatangazia watanzania wote wenye sifa kuomba kazi za Mkataba, (Vibarua) katika Ofisi za Afisa Madini Wakazi katika Mikoa ifuatayo ili kujaza nafasi wazi: Mkoa wa Dares Salaam nafasi (4 ); Katavi nafasi (2); Geita nafasi (3); Dodoma nafasi (3); Kagera nafasi (2);Kahama nafasi (2); Kigoma nafasi (2); Kilimanjaro nafasi (3); Lindi nafasi (2); Mara nafasi (3); Manyara nafasi (2); Mbeya nafasi (2); Mirerani nafasi (3); Morogoro nafasi (2); Rukwa nafasi (3); Tanga ,nafasi (2), Tabora nafasi (2), Chunya nafasi (3); Singida nafasi (3); Simiyu nafasi (2); Shinyanga nafasi (2); Ruvuma nafasi (2); Mwanza nafasi (3); Mtwara nafasi (2); na Arusha nafasi (2).
Sifa za Mwombaji i. Mwombaji awe amehitimu na kufaulu elimu ya kidato cha Nne; ii. Mwenye Cheti kutoka Chuo cha Madini; au iii. Cheti cha uhasibu au ugavi kutoka chuo chochote kinachotambulika na Serikali; na iv. Umri usiozidi miaka 45.
Kazi za kufanya a. kukagua na kudhibiti matumizi ya Hati za Mauzo ya madini ya Ujenzi; b. Kukagua magari yanayobeba madini ya ujenzi, na kukusanya Hati za Mauzo kutoka kwa wasafirishaji wa Madini ya Ujenzi; c. Kuweka kumbukumbu za taarifa za ukaguzi wa magari yanayopita kituoni ikiwemo aina ya madini, idadi ya madini; d. Kutoa taarifa zinazohusu ukaguzi wa madini ya ujenzi kwa Msimamizi wako kuhusiana na kazi zako za kila siku; e. Kutambua uhalali wa lakiri katika vifurushi au chombo kilichobeba madini au sampuli za madini yanayosafirishwa kwenda nje au kuingizwa ndani ya nchi na pia, kurekodi uzito na taarifa mbalimbali juu ya madini au sampuli hizo; f. Kufanya ukaguzi wa mizigo na uthibitishaji ( pale inapobidi ) madini au sampuli ya madini yanayosafirishwa nje au kuagizwa; g. Kufanya ukaguzi wa pamoja na maafisa wengine wa mamlaka tofauti juu ya uhalali wa nyaraka za kuagiza na kusafirisha madini nje ya nchi ikijumuisha vibali, leseni, ankara ; h. Kuzuia na kushikilia madini yoyote au sampuli ya madini katika milki ya mtu yeyote asiyekuwa na kibali cha kuyamiliki ( muuzaji / broker au mfanyakazi yoyote asiyekuwa na kibali) na kuyawasilisha kwa Tume ya Madini kwa hatua Zaidi; i. Kukusanya vibali vyote vya kusafirishia madini kutoka kwa Postmaster au Afisa wa Forodha na kuvikabidhi kwa Afisa mwenye mamlaka ya kuvitunza; j. Kutoa taarifa juu ya mtu yeyote anayehisiwa kusafirisha madini au sampuli ya madini bila kibali na kumshikilia mtu huyo chini ya ulinzi kwa kushirikiana na Maafisa wa Forodha na Polisi na;
k. Kujaza ripoti ya kila siku na kutuma kwa msimamizi wako kwa njia ya Nukushi au barua pepe kila wiki.
Mshahara kwa Mwezi Kwa waombaji watakaofanikiwa kuajiriwa ajira ya Mkataba, Mshahara kwa Mwezi Shilingi 500,000/= Ajira hii ni ya Mkataba wa Miezi mitatu.
Utaratibu wa Kuomba Waombaji wote wawasilishe maombi yao ya kazi kupitia Anwani zifuatazo:-

Afisa Madini Mkazi, Ofisi ya Madini Dar es Salaam, S.L.P. 3060, DARES SALAAM
Afisa Madini Mkazi, Ofisi ya Madini Katavi, S. L. P. 75, MPANDA-KATAVI
Afisa Madini Mkazi, Ofisi ya Madini Kahama, S.L.P. 26, KAHAMA
Afisa Madini Mkazi, Ofisi ya Madini Morogoro, S.L.P. 601, MOROGORO
Afisa Madini Mkazi, Ofisi ya Madini Geita, S.L.P. 26, GEITA
Afisa Madini Mkazi, Ofisi ya Madini Kigoma, S.L.P. 268, KIGOMA
Afisa Madini Mkazi, Ofisi ya Madini Mirerani, S.L.P. 5044, MIRERANI
Afisa Madini Mkazi, Ofisi ya Madini Tanga, S.L.P. 5153, TANGA
Afisa Madini Mkazi, Ofisi ya Madini Chunya, S.L.P. 81, CHUNYA
Afisa Madini Mkazi, Ofisi ya Madini Dodoma, S.L.P. 903, DODOMA
Afisa Madini Mkazi, Ofisi ya Madini Rukwa, S.L.P.573, RUKWA
Afisa Madini Mkazi, Ofisi ya Madini Tabora, S.L.P. 1345, TABORA
Afisa Madini Mkazi, Ofisi ya Madini Mwanza, S. L. P. 1035, MWANZA
Afisa Madini Mkazi, Ofisi ya Madini Kagera, S. L. P. 1331, KAGERA
Afisa Madini Mkazi, Ofisi ya Madini Singida, S.L.P. 925, SINGIDA
Afisa Madini Mkazi, Ofisi ya Madini lindi, S. L. P. LINDI
Afisa Madini Mkazi, Ofisi ya Madini Shinyanga, S. L. P. 834, SHINYANGA
Afisa Madini Mkazi, Ofisi ya Madini Mbeya, S. L. P. 760, MBEYA
Afisa Madini Mkazi, Ofisi ya Madini Kilimanjaro, S. L. P. 6438, KILIMANJARO
Afisa Madini Mkazi, Ofisi ya Madini Arusha, S. L. P. 641, ARUSHA
Afisa Madini Mkazi, Ofisi ya Madini Manyara, S. L. P. 500, MANYARA
Afisa Madini Mkazi, Ofisi ya Madini Ruvuma, S. L. P. 327, RUVUMA
Afisa Madini Mkazi, Ofisi ya Madini Mtwara, S. L. P. 685, MTWARA
Afisa Madini Mkazi, Ofisi ya Madini Mara, S. L. P. 785, MARA
Afisa Madini Mkazi, Ofisi ya Madini Simiyu, S. L. P. 270, SIMIYU

Waombaji wenye sifa wataitwa kupitia anwani zao za maombi ya kazi/ Namba za simu ya mkononi kwa ajili ya usaili.
Mwisho wa Kupokea maombi ni tarehe 12 Juni,2019

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*