HESLB: MAMBO YA KUZINGATIA KWA WANAFUNZI WANAO OMBA MKOPO 2019

HESLB inawakumbusha wanafunzi wanaotarajia kuomba mikopo ya shahada ya kwanza kuzingatia mambo yafuatayo:

 1. Kuwa na nakala za vyeti vifuatavyo vilivyothibitishwa na Wakili, Hakimu:
  1. Cheti cha Kidato cha Nne;
  2. Cheti cha Kidato cha Sita;
  3. Cheti cha Stashahada (Diploma);
  4. Cheti cha kuzaliwa
  5. Cheti cha kifo cha mzazi au wazazi.

Nakala za vyeti (d na e) ziwe zimethibitishwa na Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA) au Wakala wa Usajili wa Matukio ya Kijamii Zanzibar.

 1. Aidha, Wanafunzi wenye ulemavu au wenye wazazi wenye ulemavu wanapaswa kuwa na barua zinazothibitisha ulemavu huo kutoka kwa Mganga Mkuu wa Mkoa, Wilaya au Kituo cha Afya cha Serikali;
 2. Wanafunzi ambao walifadhiliwa masomo yao katika ngazi ya Sekondari au Stashahada (Diploma) wawe na barua za uthibitisho wa udhamini huo kutoka katika taasisi zilizogharamia masomo yao;
 3. Waombaji wote wa mikopo wanakumbushwa kuusoma kwa makini mwongozo wa 2019/2020 na kuuzingatia.

Kwa maelezo zaidi, tuandikie kwa

Baruapepe: adcp@heslb.go.tz

Kuupakua mwongozo 1. KWA KISWAHILI BOFYA HAPA.
2. IN ENGLISH CLICK HERE.

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*