HESLB: KOZI AMBAZO ZIMEPEWA VIPAUMBELE KATIKA KUPEWA MKOPO 2019

MAKUNDI YA PROGRAMU
makundi ya programu zifuatazo zenye vipaumbele zitapewa mikopo kulingana na uwepo wa fedha.

KUNDI LA KWANZA
Kozi katika kundi la kwanza ni: –
(i) Ualimu wa Sayansi (Fizikia, Kemia na Baiolojia) na ualimu wa hisabati na masomo ya biashara na Shahada ya uzamili katika Uhandisi wa Ndege na matengenezo
(ii) Sayansi za afya (Udaktari, upasuaji meno, madawa ya mifugo, Ufamasia, Uuguzi, Ukunga, shahada ya sayansi katika Prosthetikia na Mifupa, Shahada ya sayansi katika Mazoezi ya viungo, Shahada ya sayansi ya afya na maabara, Shahada ya sayansi ya maabara na matibabu na shahada ya sayansi ya Teknolojia ya mionzi.
(iii) Programu za Uhandisi (Ujenzi, Mitambo, Umeme, Uchimbaji Madini, Utengenezaji nguo, Kemikali na matayarisho, kilimo, Chakula na matayarisho, Automobile, Viwanda, Umeme na elekroniki, Legal and Industrial Metrology, Usafiri majini, Teknolojia ya uhandisi wa baharini, Elektronikia na mawasiliano, kompyuta, programu za sayansi ya kompyuta, habari na mitandao, Mazingira, na Mipango miji, usindikaji na huduma baada mavuno
(iv) Jiolojia ya petroli, kemia ya petroli
(v) Kilimo, Misitu, Sayansi ya wanyama na Usimamizi wa uzalishaji

 

KUNDI LA PILI
Kozi katika kundi hili ni:
(i) Programu za msingi za sayansi (shahada ya sayansi kwa ujumla katika wanyama, mimea, kemia, fizikia, Baiolojia, baiolojia ya viumbe vidogo, baiolojia ya mifugo na Bioteknolojia, Uvuvi na mifugo, Sayansi ya mazingira na uhifadhi, Matibabu, Hisabati na takwimu, Sayansi ya mazingira na usimamizi, Afya na mazingira, Baioteknolojia na maabara, Wanyamapori na uhifadhi, na Kompyuta); Tehama, vipimo na mizani, mazingira na maendeleo ya miji.
(ii) Programu ya sayansi ya ardhi (Ubunifu majengo, Ubunifu mandhari nje ya majengo, usanifu ndani ya majengo, Uchumi ujenzi, Mipango miji na vijiji, Usimamizi na uthaminishi ardhi, Jiospasho, Teknolojia katika usanifu).

 KUNDI LA TATU
Programu katika kundi hili ni pamoja na Biashara na Uongozi, Sayansi za jamii, Sanaa, sheria, lugha, fasihi na masomo ya uandishi wa habari na mawasiliano. Programu zingine zote ambazo hazijaorodheshwa katika makundi mengine zitaangukia katika kundi hili la tatu. Shahada zingine zote ambazo hazikutajwa kwenye kundi la kwanza, la pili au la tatu zitajumuishwa katika kundi la tatu.

DOWNLOAD PDF FILE-KUFAHAMU ZAIDI

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*