
WITO WA KUJIUNGA NA MAFUNZO YA JKT MUJIBU
WA SHERIA AWAMU YA TATU MWAKA 2019.
Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) limetangaza awamu ya tatu ya orodha ya majina ya vijana waliohitimu elimu ya sekondari kidato cha sita kwa mwaka 2019, kutoka shule mbalimbali za Tanzania Bara kuhudhuria mafunzo ya JKT kwa Mujibu wa Sheria.
Sanjari na uchaguzi huo, JKT limewapangia vijana hao, makambi ya JKT watakayokwenda kupatiwa mafunzo kwa muda wa miezi mitatu na wanatakiwa kuripoti makambini kuanzia tarehe 26 June 2019 hadi tarehe 05 Julai 2019.
Aidha, wahitimu wenye ulemavu wa kuonekana kwa macho, (physical disabilities) wanatakiwa kuripoti kambi ya JKT Ruvu iliyopo eneo la Mlandizi mkoani Pwani ambayo imejengewa miundombinu ya kuhudumia watu wa jamii hiyo.
Mkuu wa JKT, anaendelea kuwakaribisha vijana wote waliochanguliwa ili waweze kuungana na vijana wenzao katika kujifunza uzalendo, umoja wa kitaifa, stadi za kazi, stadi za maisha na utayari wa kulijenga na kulitumikia Taifa letu.
Orodha kamili ya majina ya vijana waliochanguliwa awamu ya tatu, maeneo ya makambi ya JKT waliyopangiwa na vifaa wanavyotakiwa kwenda navyo inapatikana katika tovuti ya JKT ambayo niĀ www.jkt.go.tz
KUONA MAJINA HAYO BOFYA HAPO CHINI
Imetolewa na:
Kurugenzi wa Habari na Uhusiano
Makao Makuu ya JKT
Tarehe 25 Juni 2019
Leave a Reply