NAFASI YA KAZI KATIKA OFISI YA MWANASHERIA MKUU ZANZIBAR

Tume ya Utumishi Serikalini inatangaza nafasi za kazi kwa ajili ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu Zanzibar kama ifuatavyo:-

1. Wakili wa Serikali Daraja la II “Nafasi 8”
SifazaWaombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu elimu ya Shahada ya kwanza ya Sheria kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
• Awe anaweza kuendesha mashtaka kwa uadilifu na uaminifu.

2. Afisa Utumishi Daraja la II “Nafasi 1”
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu Shahada ya Kwanza katika fani ya Utawala wa Umma au Rasilimali Watu kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

3. Muhudumu Daraja la III “Nafasi 1”
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amemaliza elimu ya Sekondari.

4. Dereva Daraja la III “Nafasi 2”
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu Elimu ya Sekondari na kupata Mafunzo ya Udereva na leseni hai ya Udereva kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

5. Walinzi Daraja la III “Nafasi 3”
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amemaliza elimu ya Sekondari.
• Awe amepata Mafunzo ya Ulinzi (Mgambo au JKU au JKT)

6. Katibu Muhtasi Daraja la III “Nafasi 4”
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu Stashahada katika fani ya Uhazili kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

7. Mwangalizi wa Ofisi Daraja la III “Nafasi 1”
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu Stashahada katika fani ya Utawala wa Umma au Rasilimali Watu kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

8. Karani Sheria Daraja la III “Nafasi 2”
SifazaWaombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu elimu ya Stashahada ya Sheria kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

9. Afisa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano Daraja la II “Nafasi 2
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu Shahada ya Kwanza katika fani ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (ICT) kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

10. Taarishi Daraja la III “Nafasi 1”
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu elimu ya Sekondari.

Jinsi ya Kuomba:
• Barua za maombi ziandikwe kwa Mkono na zitumwe kwa anuani ifuatayo:-
KATIBU,
TUME YA UTUMISHI SERIKALINI,
S. L. P 1587 – ZANZIBAR.

• Muombaji anaombwa kuwasilisha ombi lake moja kwa moja katika Ofisi ya Tume ya Utumishi Serikalini iliyopo Jumba la Wananchi Forodhani Zanzibar wakati wa saa za kazi. Kwa waombaji walioko Pemba wanaombwa kuwasilisha maombi yao Ofisi ya Rais, Utumishi wa Umma na Utawala Bora Chake Chake Pemba.

Barua za Maombi ziambatanishwe na mambo yafuatayo:-
a) Kivuli cha Cheti cha kumalizia masomo
b) Kivuli cha Cheti cha mtihani wa Taifa (Elimu ya Sekondari)
c) Kivuli cha Cheti cha Kuzaliwa.
d) Kivuli cha Kitambulisho cha Mzanzibari.
e) Picha moja (1) ya Passport Size iliyopigwa karibuni.
f) N.B: Atakaewasilisha ‘Statement of Result’ au ‘Progressive Report’ maombi yake hayatazingatiwa.
g) Tarehe ya mwisho ya kupokea maombi ni tarehe 05 Julai, 2019 wakati wa saa za kazi

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*