WAZO LA BIASHARA : BIASHARA YA KUTENGENEZA NA KUUZA JUICE YA TENDE

WAZO LA BIASHARA

JUICE YA TENDE🥤🥤🥤

Hivi ushawahi Jiuliza Wapishi ni wengi Duniani, kuna Restaurants nyingi sana, kuna hotels nying sana Lakin UNAKUTA MAARUFU ZAIDI na watu wengi wanazozifahamu ni KFC, MacDonald, PizzaHut????

Yan Kitu wanachotengeneza ni Kile kile…lakin mtu ana Feel Proud akienda KFC😄….!! SIO UCHAWI…ILA NI BRANDING….

Unaweza ukauza ata mawe….na ukawa maarufu na ukatuboa..endapo utafanikiwa kwenye ishu ya BRANDING!!😃

Nisizungumzie sana maswala ya Branding…..embu Tuje kwenye mada yetu ya JUICE YA TENDE

Juisi ya Tende ni miongoni mwa juisi zilizojizolea umaarufu mkubwa hasa katika kurekebisha tatizo la nguvu za kiume.( Ina aminika sana hivo na jamii yetu hapa Bongo….kwasisi wajasiriamali TUNACHUKULIA KAMA OPPORTUNITY PA KOTOKEA SASA HAPO😄)

FAHAMU JINSI YANKUITENGENEZA

Huu Ni mfano wa ambao utakusaidia kuelewa jinsi ya kutengeneza:

MAHITAJI :

  • Tende kilo moja
  • Maziwa ya unga au ya ng’ombe lita moja
  •  Sukari kiasi upendacho.

MUHIMU : Tende zina asili ya sukari hivyo hakikisha unaweka kiasi

NAMNA YA KUTENGENEZA :
– Chukua tende zako kisha zitoe mbegu zake.

– Hakikisha unatoa mbegu tu na kuziacha tende kama zilivyo bila kutoa kitu kingine.

– Anza kuzisaga peke yake kwenye brenda hadi zitakapolainika  vizuri.

– Mimina maziwa yako kidogokidogo kwenye brenda ili kuzisaga vema jambo litakalosaidia juisi yako kulainika vema.

– Baada ya kutia maziwa yote na kuisaga sawasawa, tia sukari kiasi upendacho huku ukiendelea kuisaga ili sukari yako iweze kuchanganyika vizuri na juisi yako.
– Juisi yako itakuwa tayari kwa kunywa sambamba na kitafunwa chochote ukipendacho kama vile bagia, sambusa, korosho au karanga.

 

UNAFANYAJE BIASHARA HII YA JUICE YA TENDE??? kwanini JUICE YA TENDE??🥤🥤

Ndio !! Juice ya Tende…Kwasababu sio watu wengi wanafanya hii biashara……

Yan ukizungumzia Biashara ya Juice hapa Bongo….Wengi wao wanauza hizi Juice common za matunda mengine…..kwahiyo wewe unaweza kuja Kivyako na Juice ya tende tuuh!!

KUHUSU MASWALA YA MTAJI na BUDGET !! Kiukweli hapo UTAJIPIMIA MWENYEWE..mimi sio.mtaalamu sana wa maswala ya fedha😄

Sasa ishu ipo kwenye BRANDING NA UNAIFANYEJE!!

Yan, ukitaka utoboe kwenye hizi biashara za juice….Lazima UFANYE BRANDING na UWE OFFICIAL!!

Branding…..nazungumzia

● Chagua Jina Zuri, Logo, Fungua social Media Accounts za biashara yako, Fungua website, na pia Fungua MOBILE APP ya watu ambayo wanaweza ku-Order Online

● Sajili Biashara Yako

● Sehemu Quality -Ofisi, ambayo utakuwa unatengenezea & Kuuza hiyo Juice …

– Hapa ni kuchagua maeneo ambayo unajua utapata wateja (Kulingana na Wateja uliowalenga)

—->>> Watu wengi wanakimbiliaga maeneo ya Sheli za magari…..!! Ni vizur kama umetarget wateja wako ..LAKINI USIKARIRI!!!….

—->>> Biashara ya Juice unaweza fungua popote na UKAWA UNAFANYA DELIVERY KWENYE MAOFISI NA MAKAZI.MBALI MBALI!!!🚚🥤

● Usafi wa mazingira na bidhaa zako & Hakikisha ata unakuwa na Nutrianalist / Food Officer by Professional…..

– Hii itakusaidia sana kujemga uaminifu na wateja wako..kuwa unajali afya

● Packaging — Yan Packaging iwe Quality…🥤🥤….Hakikisha Umeweka JINA na LOGO kwenye Package zako…..KUWA MBUNIFU SANA MAENEO hayo !!

Hizo ni baadhi ya Basic Tips tuuh…Mambo mengine Utajiongeza!!

 

KUHUSU WATEJA……

● Tatizo watu wengi tumekuwa tukiiga na kukariri…..Yan kwakuwa umeona watu wanauza JUICE maeneo ya sheli au Car wash….nawewe unataka KUFUNGUA MAENEO HAYO HAYO…!!

—–>>>>> Embu Jaribu kuandaa Proposal & Presentation nzuri ya Biashara yako tafuta vijana wawili wanaojua Marketing vizuri……. PITENI MAOFISI MBALI MBALI hapo Mjini…Jaribu kutafuta soko uko!!!……….Pita kwenye mabenki, ofisi za makampuni mbali mbali, Pita ata kwenye maduka hapo town, Hadi Mahospitalini, Mashuleni, Ofisi za umma n.k……uwaelezee biashara yako!! Wape Offer siku mbili tatu……!! LAZIMA UTAPATA WATEJA TUUH!! TENA WATEJA WALE WA KUDUMU WA KILA SIKU KUWALETEA JUICE!!

——>>> uo ni mfano tuh, ila point ni ku- Tambua AINA YA WATEJA unaowahitaji na uwatafute!!!

Asanteni!!!

KWA MASWALI / MAREKEBISHO/ USHAURI

Wasiliana nasi

Email: unistoretz9@gmail.com

 

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*