NAFASI 20 ZA KAZI UDART-WAKALA WA MAGARI YA MWENDO KASI

NAFASI ZA KAZI UDART

Kumb Na: AB.23/134/01-G/101 17 JULAI, 2019
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka, anakaribisha maombi ya kazi kutoka
kwa watanzania wenye sifa na uwezo wa kujaza nafasi wazi ishirini na sita (26) kama
zilivyobainishwa katika tangazo hili.
MKUSANYA MAPATO (20)
SIFA ZA MUOMBAJI.
Awe na elimu ya Kidato cha nne na amehitimu elimu ngazi ya cheti katika fani zifuatazo
(Uhasibu, Biashara, Manunuzi, Takwimu, Hisabati) kutoka chuo vinachotambuliwa na Serikali.
MAJUKUMU YA KAZI.
i. Kukusanya fedha zote katika maegesho ya magari pamoja na sehemu za huduma ya choo,
ii. Kukusanya takwimu za magari yanayoegeshwa kwa siku pamoja na takwimu za watumiaji wa
choo kwa siku,
iii. Kuandaa hesabu za makusanyo ya kila siku kwa kutumia fomu za RCCB,
iv. Kutunza fedha zote za makusanyo ya siku na kuhakikisha Usalama wa fedha hizo kabla
hazijafika ofisini,
v. Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na mkuu wake wa kazi zinazohusiana na Elimu,
uzoefu na ujuzi wake.
MHUDUMU WA MAKUNDI MAALUM (6)
SIFA ZA MWOMBAJI
Awe na Elimu ya kidato cha nne na amehitimu elimu ya cheti cha mafunzo ya miaka miwili
katika fani ya maendeleo ya jamii/Ustawi wa jamii kutoka vyuo vya maendeleo ya jamii
vinavyotambuliwa na serikali
MAJUKUMU YA KAZI
i. Kutambua na kuhudumia watu walio katika makundi maalum,
ii. Kukusanya takwimu zinazohusu watu walio katika makundi maalum wanaopita katika vituo,
iii. Kutoa taarifa ya utekezaji wa kazi zake kila wiki,
iv. Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na mkuu wake wa kazi zinazohusiana na Elimu,
uzoefu na ujuzi wake.

MSHAHARA: Kima cha mshahara kwa nafasi zote ni shilingi 310,000/=
MASHARTI YA JUMLA
i. Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania,
ii. Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa,
iii. Waombaji wote wawe na umri kuanzia miaka 18 hadi 45,
iv. Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye anwani na
namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees)watatu wa kuaminika.
v. Maombi yote yaambatane na vyeti vya kidato cha nne, taaluma, kwa wale waliohitimu
mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika waambatanishe vyeti vya mafunzo
husika.
vi. Testmonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati matokeo za kidato cha nne
na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA
vii. Picha moja “Passport size” ya hivi karibuni.
viii. Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na Baraza la
Mitihani Tanzania – (NECTA).
ix. Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kugushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.
Maombi yote yatumwe kwa: –
MTENDAJI MKUU,
WAKALA WA MABASI YAENDAYO HARAKA,
S.L.P 724,
DAR ES SALAAM.
Mwisho wa kutuma maombi ya kazi ni tarehe 24 Julai, 2019.
Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu ulioainishwa katika tangazo hili
HAYATAKUBALIWA.

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*