NAFASI ZA KAZI-ELCT KKKT Dayosisisi ya Kaskazini

KKKT Dayosisisi ya Kaskazini inasimamia Hospitali tatu ambazo ni Marangu, Machame na Karatu zinazotoa huduma za afya. Katika kutoa huduma bora tunatafuta watu wa kuajiri katika nafasi zifuatazo:

AFISA MUUGUZI DARAJA LA II (NURSING OFFICERS)
Majukumu yake ni kama yafuatavyo;
 Kufanya kazi za kiuguzi hospitalini, katika jamii na sehemu zote zinazotolewa huduma za Afya pamoja na huduma kwa wagonjwa majumbani.
 Kutayarisha mpango kazi wa huduma ya uuguzi na taarifa ya utekelezaji wake
 Kukusanya takwimu muhimu za Afya
 Kutoa elimu na ushauri nasaha kwa wagonjwa na jamii
 Kutoa huduma za kinga na uzazi
 Kutekeleza majukumu mengine atakayopangiwa na mkuu wake wa kazi Sifa za Mwombaji:
 Awe na shahada ya Uuguzi kutoka Chuo Kikuu kinachotambuliwa na Serekali
 Awe amehitimu mafunzo ya vitendo kazini (Intership)
 Aliyesajiliwa na Baraza la Wauguzi na Wakunga Tanzania

MSAIDIZI WA AFYA
Majukumu yake ni kama yafuatavyo;
 Kuchukua Sampuli za maji na chakula na kuzipeleka kwa Afisa Afya Mazingira au Afisa Afya Mazingira Msaidizi
 Kutambua, kuweka kumbukumbu za vyanzo vya maji na kuhamasisha jamii kulinda vyanzo vya maji kwa kushirikiana na kamati za maji za vijiji na mitaa
 Kutoa elimu kwa jamii kuhusu usafi, kudhibiti taka hatari/hatarishi zikiwamo zitokanazo na huduma za afya na kuhamasisha jamii kujenga na kutumia vyoo bora
 Kufanya ukaguzi wa nyumba za kuishi na za biashara
 Kusimamia sheria ndogo ndogo za afya na mazingira
 Na kazi nyingine atakazopangiwa na mkuu wake wa kazi

Sifa za Mwombaji:
 Awe amehitimu kidato cha nne
 Awe na cheti cha mafunzo ya Msaidizi wa Afya au Fundi Sanifu Afya na Mazingira toka kwenye Chuo kinachotambuliwa na Serikali Watakaopenda watume maombi yao pamoja na picha ndogo ya karibuni (recent passport size) pamoja na wasifu wao (Curriculum Vitae) kwa Anuani ifuatayo kabla ya tarehe 10/08/2019:

Katibu Mkuu
KKKT Dayosisi ya Kaskazini
S.L.P 195,
MOSHI
Barua pepe: generalsecretary@northerndiocese.co.tz

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*