Wanafunzi kumi bora wavulana matokeo darasa la saba watoka kanda ya ziwa

Dar es Salaam. Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) limetangaza matokeo ya kumaliza elimu ya msingi mwaka 2019 ambapo asilimia 81.50 ya watahiniwa 933,369 wamefaulu mtihani huo huku watahiniwa 909 wakifutiwa matokeo kwa sababu ya udanganyifu.

 

Akitangaza matokeo hayo  leo Jumanne Oktoba 15, 2019 Katibu Mtendaji wa NECTA, Dk Charles Msonde amesema kwa jumla yanaonyesha ufaulu umeongezeka kwa asililia 3.78 lakini ufaulu katika somo la Kiingereza bado ni mdogo likilinganishwa na masomo mengine.

“Ufaulu katika somo la Kiingereza unaendelea kuimarika mwaka hadi mwaka hivyo juhudi za makusudi zinahitajika kuendelea kufanyika ili kuinua kiwango cha ufaulu katika somo hili,” amesema Dk Msonde.

 

Aidha katika matokeo hayo, Grace Imori Manga wa shule ya msingi Graiyaki ya mkoani Mara ametangazwa kuwa wa kwanza kitaifa akifuatiwa na Francis Gwani wa shule ya msingi Paradise ya mkoani Geita na namba tatu imeshikiliwa na Loi Kitundu wa Shule ya msingi Mbezi ya Dar es Salaam.

Katika matokeo hayo yaliotangazwa leo Jumanne Oktoba 15, 2019 nafasi ya kwanza hadi ya 10 katika orodha ya wavulana waliofanya vizuri zimeshikwa na wanafunzi kutoka katika mikoa ya kanda ya ziwa.

Nafasi ya kwanza imekwenda kwa Francis Gwaji kutoka shule ya Paradise ya mkoa wa Geita, wakati nafasi ya pili hadi ya nne ilichukuliwa na wanafunzi wa shule ya Graiyaki ya Mara ambao ni Victor Godfrey, Aziz Yassin na Goldie Hihayuma.

Nafasi ya tano imeshikwa na Daniel Daniel wa shule ya Little ya Shinyanga huku nafasi ya sita ikichukuliwa na Hilary Nassor wa shule Peaceland ya Mwanza.

Bado mikoa ya kanda ya ziwa imeendelea kutesa katika nafasi ya saba ambayo imeshikiliwa na Mbelele Mbelele wa Kwema Modern iliyopo Shinyanga, nafasi ya nane ikishikwa na Derick Lema wa shule ya Musabe mkoani Mwanza.

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*