”Kidato cha Tano wapya hairuhusiwi kuhama”- Serikali

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe Selemani S. Jafo (Mb), amesema haita ruhusiwa kwa wanafunzi waliochaguliwa kujiunga kidato cha tano mwaka 2019 katika shule mbali mbali nchini kuhama hadi muhula wa kwanza wa masomo utakapo kamilika huku zoezi hilo likitegemea uwepo wa nafasi katika shule mwanafunzi anayotaka kuhamia.

Waziri Jafo ametoa kauli hiyo akiongea na waandishi wa habari mwishoni mwa juma jijini Dodoma, wakati akitoa taarifa kuhusu uchaguzi wa wanafunzi waliofaulu na kuchaguliwa kujiunga na kidato cha Tano pamoja na Vyuo vya kati kwa mwaka wa 2019.

“Nitumie fursa hii kutahadharisa, Mabadiliko yoyote hayataruhusiwa kabla yakukamilika kwa muhula wa kwanza wa msomo na zoezi hilo litafanyika kwa kuzingatia uwepo wa nafasi kwenye Shule kwa idhini ya Maafisa Elimu wa Mikoa husika” alisema Jafo.

Jafo pia aliwataka wanafunzi hao waliopangwa kidato cha Tano kuripoti ndani ya siku 14 katika shule husika kuanzia tarehe 08 Julai, 2019 na endapo mwanafunzi atashindwa kutekeleza maagizo hayo atakuwa amejiondoa na nafasi yake itajwazwa na mwanafunzi mwingine aliyekosa nafasi.

Aidha upande wa wanafunzi wanatarajia kujunga na vyuo vya kati, Waziri Jafo alisema wametakiwa kuanza kuthibitisha kuanzia tarehe, 9 Juni hadi 30 Agosti, 2019 huku wale watakao hitaji kubadili kozi zao alisema zoezi hilo litaanza tarehe 10- Agosti, 2019 kupitia mtandao wa NACTE.

Sambamba na maelekezo hayo, Waziri Jafo, alisema jumla ya wanafunzi wavulana 1,861 waliokuwa na sifa zakujiunga na kidato cha Tano na Vyuo vya Ufundi, lakini wamekosa nafasi watapangiwa katika chagua la pili la zoezi hilo.

Takwimu zinaonesha ufaulu wa watahiniwa wa kidato cha Nne kwa mwaka 2018 kuanzia daraja la kwanza hadi la tatu ni 113,325 (wasichana 47,779 na wavulana ni 66,046 sawa na asilimia 31.76 ya watahiniwa wote waliofanya mitihani ambapo ufaulu umepanda na kwa asilimia 1.76 ikilinganishwa na mwaka wa 2017.

Anaandika Atley Kuni- TAMISEMI Dodoma

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*