UDSM : MATOKEO YA USAHILI WA AWAMU YA KWANZA (APTITUDE TEST) YA KAZI YA MUDA MFUPI YA SABASABA ULIOFANYIKA TAREHE 08 JUNI 2019

Uongozi wa Kitengo cha Kompyuta cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UCC), unapenda kuwataarifu waombaji wa kazi ya muda mfupi Sabasaba (43rd DITF) walioshiriki katika usaili (Aptitude Test) uliofanyika tarehe 08 Juni, 2019 yafuatayoo:-

  1. Watahiniwa 917, kati ya 1,195 walioitwa, walishiriki usaili wa tarehe 08 June 2019.
  2. Watahiniwa 164 (jinsia ya kiume 80, jinsia ya kike 84) ndio waliochaguliwa. Kwa jinsia ya kiume kiwango cha chini cha waliochaguliwa ni waliofaulu kwa asilimia 68, na kwa jinsia ya kike ni asilimia 60.
  3. Watahiniwa waliofaulu katika usaili wa awamu ya kwanza wanaombwa kuhudhuria usaili wa awamu ya pili (Oral Interview) utakaofanyika siku ya Jumamosi tarehe 15 Juni 2019 UCC makao makuu yaliyopo Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Mlimani Campus) Mwalimu J.K. Nyerere.
  4. Majina na ratiba ya usaili kwa kila mtahiniwa unapatikana katika kiambatanishi (Pakua hapa chini kuona majina na ratiba ya usaili).


Tafadhali zingatia yafuatayo:-

  1. Kila mtahiniwa anaombwa kuja na kitambulisho, kwa ajili ya utambuzi;
  2. Kila mtahiniwa anaombwa kuja na VYETI HALISI vya taaluma.

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*