TANGAZO LA KUITWA KUCHUKUA MIKATABA YA KAZI YA MUDA MFUPI YA SABASABA SIKU YA ALHAMISI TAREHE 20 JUNI 2019 KWA WALIOFAULU USAILI WA PILI (ORAL INTERVIEW) ULIOFANYIKA TAREHE 15 JUNI 2019.

Uongozi wa Kitengo cha Kompyuta cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UCC), unapenda kuwataarifu waombaji wa kazi ya muda mfupi Sabasaba (43rd DITF) walioshiriki katika usaili wa awamu ya pili (Oral Interview) uliofanyika tarehe 15 Juni, 2019 kama ifuatavyo:-

  1. Jumla ya watahiniwa 164 (jinsia ya kiume 80 na ya kike 84) walialikwa kushiriki katika usaili. Kati ya hao watahiniwa 156 walishiriki katika usaili na watahiniwa 8 (jinsia ya kiume 4 na ya kike 4) hawakujitokeza katika usaili.
  2. Jumla ya watahiniwa 100 (jinsia ya kiume 42 na ya kike 58) ndio waliofanikiwa kuvuka kiwango cha chini cha ufaulu (Cut off point). Kwa jinsia ya kiume cut off point ni asilimia 67, na ya kike ni asilimia 60. Kutokana na sababu mbalimbali zinazoweza kujitokeza kuhusiana na waliochaguliwa, watahiniwa 10 (jinsia kiume 5 na ya kike 5) wamechaguliwa kuwa katika orodha ya ziada (Reserve List), na watahiniwa hawa ni kati ya wale waliofuatia kwa ufaulu.
  3. Majina 100 yaliyoambatanishwa hapo chini wanaombwa kufika katika Kitengo cha Kompyuta cha Chuo kikuu cha Dar es Salaam, Mlimani Campus siku ya Alhamisi ya tarehe 20 Juni, 2019 kuanzia saa 4:00 asubuhi mpaka saa 10:00 jioni kuchukua mikataba yao ya kazi na watatakiwa kuirudisha kabla ya siku ya Jumatatu ya tarehe 24 Juni 2019.

Pakua hapa chini kuona majina ya walioitwa kazi ya muda mfupi.

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*