NAFASI 9 ZA KAZI TUME YA UTUMISHI WA MAHAKAMA

Tume ya Utumishi wa Mahakama ni chombo kilichoundwa kwa mujibu wa aya ya 112(1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977. Aidha,Sheria ya Uendeshaji waMahakama Na. 4/2011 inaipa Tume ya Utumishi wa Mahakama jukumu la kuajiri watumishi wa kada mbalimbali wa Mahakama pamoja na majukumu yake mengine.Hivyo, Tume ya Utumishi wa Mahakama inawatangazia Watanzania wenye sifa zilizoainishwa hapa chini kwa kila nafasi ya kazi na ambao wako tayari kufanya kazi katika Mahakama ya Tanzania katika Mikoa mbalimbali kuleta maombi yao ya kazi.Nafasi hizo ni Mkaguzi wa Hesabu wa Ndani Daraja la II –(TGS. D)nafasi 1,Mhasibu Daraja la II TGS D nafasi 1 na Mhasibu Msaidizi (TGS C)nafasi 2, Mhandisi Daraja la II TGSEnafasi 2, Msanifu Majengo (Architect) Daraja la IITGSEnafasi 1na Mkadiriaji Ujenzi (Quantity Surveyor) Daraja la IITGSEnafasi 2

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*