ELIMU YA BIASHARA: FAHAMU KUHUSU HUDUMA KWA WATEJA(JINSI YA KUHUDUMIA WATEJA WAKO)

CUSTOMER CARE. (HUDUMA KWA WATEJA)
Kama kuna sehemu wafanyabiashara wengi ndani ya nchi hii wanakwama ni kwenye eneo la Huduma kwa wateja ( CUSTOMER CARE!! )
Sehemu nyingi ukienda utoaji wa huduma kwa wateja ni zero. Kuna watu wanauza vyakula kuanzia uhudumiaji, mapokezi, mpaka kupata huduma yenyewe ni zero, kuna watu wana saloon hawajui kabisa kuhudumia wateja na wafanyabiashara wengine wengi, huduma kwa wateja ni tatizo.
Mfanyabiashara kuna mambo unapaswa kuyafahamu;
1. Tupo kwenye dunia iliyojaa ushindani( competitive world) kwa kasi ya ushindani huu unahitaji kuwa Mbunifu kwenye kila jambo, hasa kwenye huduma kwa wateja.
2. Mteja wako ni Balozi, anaweza kuwa balozi mbaya au mzuri itategemeana na ulivyomhudumia.
3. Hakuna biashara pasipo watu, huduma zako zinaweza kuwabakisha au kuwafukuza.
Yafuatayo ni Maeneo muhimu ya kuzingatia kwenye Huduma kwa wateja.
LUGHA;
Hii ni nyenzo ya muhimu sana, inaweza kujenga au kubomoa kutegemeana na itakavyotumika. Je unawakaribisha vipi wateja? Unawahudumia vipi? Wanapokukosoa unawajibu vipi?
Jitahidi sana kuwa na lugha nzuri, inapobidi omba samahani, karibisha wateja wako kwa tabasamu na maneno mazuri, waonyeshe vile unawathamini na kuwapenda.
N.B
Kwenye kupamba lugha , usitie chumvi nyingi mpaka ukawa muongo, UAMINIFU ni mtaji mkubwa sana.
Kiuhalisia, hakuna binadamu asiyependa kuthaminiwa, wathamini watu kwa lugha nzuri uone kama biashara yako haitastawi.
.
. *ITAENDELEA* ©AMINA SANGA.

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*