WAZO LA BIASHARA !! TENGENEZA ZAIDI YA LAKI.5 KWA WEEK, KWA BIASHARA HII YA MASHINE YA KUFULIA(LAUNDRY BUSINESS)

MASHINE YA KUFULIA INALIPA……… !!!

KUNA WATU WANATENGENEZA ZAIDI YA 500,000Tshs kwa week!!

Kuna siku katika harakati zangu nliingia Bank flan kufungua account….. Nlipenda huduma ya pale Bank kiasi kwamba hadi yule aliyekuwa ananihudumia akawa kama rafiki yangu…Huku anaendelea kunihudumia,…. alikuwa anaongea sana na wafanya wake pamoja namimi……

Katika zile story zake zote nlisikia jamaa akilalamika Kuwaambia wenzake kuwa “YULE JAMAA ANAYECHUKUAGA NGUO, WEEK HII HAKUJA”…. na wenzake pia walikuwa wanalalamika icho kitu!!!….. Yule jamaa akaniuliza kuna sehemu ingine wanatoa huduma kama hiyo iyo…Kama naifahamu??…(YANI MASHINE YA KUFULIA)….kiukweli mimi mwenyewe nlikua sijui..!!

Na ndipo WAZO LIKANIJIA HAPO HAPO KUMBE HII NAYO NI BIASHARA NA WATU WANAPIGA PESA!! 😅

Kwamaana jamaa aliniambia analipia elfu.10 kila week na wako kama 5 hapo kazini…yan uyo jamaa anawafataga kila weekend kuchukua nguo……!!

Nlijaribu kutafuta mtu anayefanya biashara kama hiyo…kwa maeneo nlipo , nliulizia nkikosa!!..Ila nlipewa na namba ya mtu anayefanya biashara kama hiyo Dar……

Nliwasiliana nae uyo jamaa , kiuweli naweza kusema alinifungua sana na aliniambia baadhi ya mambo ambayo ningependa kushea hapa Kuhusu hii biashara!!!!…..

 

Jamaa aliniambia hii biashara watu wengi bado hawajashtuka!! Na ata ambao wachache wanaifanya…Hawajui jinsi ya kuifanya..!!!..

UZURI WA HII BIASHARA…UKIPATA WATEJA, YAN WATEJA WAKO NI HAO HAO WA KUDUMU MILELE😄

Huwa napenda kusema Kila biashara Inalipa , Ishu ipo ni UNAIFANYAJE ??? Na Utapataje wateja???

Bei ya mashine ya Kufulia …zipo za AINA NYINGI……

Yani bei inaanzia kuanzia 500K hadi Million 1 au zaidi….. Ila nyingi nlizoana bongo…nuzri wanauza 900K Tshs!!

Sasa embu tuashumu wewe umenunua ile bora kabisa ya 1M Tshs na umepata ofisi /frame nzuri kila kitu kwa bajeti yako unayoijua mwenyewe…

Ishu ipo kwenye kutafuta WATEJA!!!..

Image result for laundry business

 

Zingatia mambo haya!!

Mimi nlishaongeleaga swala la Branding…..Hakikisha Ume brand Biashara yako ni iwe Official….!! USIFANYE VITU KIENYEJI enyeji’,…. ( Biashara yako iwe na Jina, Logo, documentation, Mikataba, usajili, Ofisi, social Media Accounts n.k) & PROMOTE YOUR BUSINESS

● Kwa teknolojia inavyokuwa unaweza pia kutengeneza Mobile app…ambayo.mtu anaweza ku -Book au kuweka order…. Online!!

● Tambua, aina ya wateja wako ni watu wa aina gani….. WATU WANAOPENDA KUTUMIA HIZO, wengi wao ni wale mabachelor na wako busy !! Au watu wale wanaoshindaga maofisini

Sasa hapa kwenye kutafuta wateja…..unahitaji ORDER ZA WATU 50 tuuh kutengeneza Laki.5 kwa week!!!

Kama kweli utaweza kutafuta Wateja…..ambao unajua ukilenga maofisi flan au majumba flan Huwezi kosa watu watakayohitaji huduma hiyo!!!……

Sasa achana na kutafuta watu….KUNA HIZI LODGE, GUEST NA MAHOTELI!!!

yan ukifanikiwa Kupata GUEST ZAKO kama 20 hivi…uwe unaenda kuchukua Nguo kule au LODGE au Mahoteli…bhasi hapo ni uhakika wa WATEJA WA KUDUMU!!!

huyo jamaa ndio kitu anachofanya sasa…. yeye anakwambia aliwatafuta hawa wamiliki wa magest House kama 50 hivi…alibahatisha hapo kupewa tender za Kufulia Gesti kama 32 !!..na anakwambia saivi ana tender ya hotels kama 8 tayar….!! Yeye kazi yake ni Huduma ya Kufua tuh!!…kwahiyo wanaenda kuchukua Nguo na nakuzirudisha !!

Sasa kama ana guest moja..anakwambia anaweza wapangia Bei ata 30K Kwa week  kila gest/lodge!! Na anawafulia kila siku..ila anachukua 30K yake kila week na zipo gest kama 30….means anapata kiasi kizuri na ni uhakika..kwamaana AMEINGIA NAO MKATABA😃😃…… hapo bado kuna wale watu wake wanao order kufuliwa……uhakika kwake minimum sio chini ya LAKI.5 kwa week FAIDA..!!

Sio kazi rahisi kufikia level hiyo…lakini kila kitu kinawezekana…. Ishu ipo kwenye kupata hizo TENDER ZA MAHOTEL /GUEST/LODGE na WATU….

Mimi lengo langu ni kuleta WAZO LA BIASHARA tuuh…so kazi kwako kama umelipenda na kuanzia kulifanyia kazi!!

Asanteni!!

© Imeandaliwa na Kuandikwa na Unistoretz Inc

Kwa maoni na Ushauri wasiliana nasi

unistoretz9@gmail.com

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*